Majadiliano ya Bodi ya Kusimamia na Kuendesha Ligi, kiliketi mwanzoni mwa wiki hii
na kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyotokea kwenye michezo
mbalimbali ya mpira wa miguu kwa michuano yote – Ligi Kuu ya Vodacom,
Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.
Haya haya ndiyo yaliyojiti katika kila mchezo.
Mechi namba 170 (Stand United FC vs Majimaji).
Majimaji iliwasilisha malalamiko kuwa chumba chao kubadilishia nguo
(changing room) kilipuliziwa na timu pinzani dawa ambayo ni sumu, hivyo
kushindwa kukitumia wakati wa mapumziko.
Klabu
ya Stand United FC pamoja na Meneja wa Uwanja waandikiwe barua kuwa
vitendo hivyo vikiendelea kujitokeza uwanja huo utafungiwa kwa mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom.
Msimamizi wa Kituo aandikie taarifa yake (report) kuhusu tukio hilo. Pia Daktari wa Uwanja, Dk. Abel Kimuntu awasilishe taarifa yake ya kitaalamu kuhusu suala hilo, vilevile Meneja wa Uwanja huo, Meja mstaafu Mohamed Ndaro naye awasilishe taarifa yake kuhusu tuhuma hizo za kumwaga dawa kwenye vyumb