Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezindua mradi wa maji katika kijiji cha
Mkola Kata ya Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya uliogharimu
zaidi ya shilingi milioni mia tatu tisini na saba.Akifungua mradi huo
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa Wilaya zote mkoaani Mbeya kuwaondoa watu
wote waliovamia vyanzo vya maji.Hata hivyo Makalla amewataka wananchi
wa Mkola kuutunza mradi huo na kuhamisha uwanja wa mpira ili chanzo
hicho kisiingiliane na shughuli za kibinadamu. Akisoma taarifa mbele ya
Mkuu wa Mkoa mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema ujenzi wa
Mradi huo umeanza mwaka 2009 kwa ushirikiano baina ya wananchi,
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na Serikali Kuu. Naye Mkurugenzi
mtendaji Sophia Kumbuli amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya kwa
kushirikiana na wananchi wa Mkola watatafuta eneo la kuhamishia uwanja
wa mpira Halmashauri itatoa tingatinga kwa ajili ya kusawazisha. Mradi
huo mpya utanufaisha zaidi ya wananchi elfu na maji yake hapana magari .
Kwa upande wao wananchi wameushukuru serikali kwa kukamilisha mradi huo
na kuahidi kuutunza ili kuondoa changamoto iliyokuwa inawakabili.