Dk 75, Bocco anaachia mkwaju mkali wa adhabu, unamtoka Agyei halafu anadaka tena
Dk 72 Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya Mavugo kuikosa krosi safi ya Ajibu
Dk 68, Himid anaachia mkwaju mkali wa mpira wa Adhabu, Kichuya anaweka kichwa na unaokolewa
Dk 66, Manula anaonyesha umahiri akipangua shuti kali la Ajibu, sentimeta chache kutoka katika lango lake, inakuwa kona ya tano ya Simba, inachongwa na kuokolewa
Dk 65 sasa, mpira kama umepoa hivi, Azam FC wanaonekana kuwa makini zaidi katika ulinzi
Dk 61, Mo Ibra anatoa pasi nzuri kwa Mavugo, anaachia shuti kali, mpira unatoka sentimeta chache kidogo nje ya lango la Azam FC...ilikuwa hatari
Dk 61 Kichuya nje ya 18 anaachia shuti lakini linatoka nje
Dk 60 sasa, Simba wanaanza kuonekana kama wamepoteza ile hali ya umakini na kucheza kitimu
SUB Dk 58 anaingia Joseph Mahundi kichukua nafasi ya Kingue, sasa Azam FC wanataka kufunga na huenda wakatumia mipira ya mashuti kupitia kiungu huyu aliyeingia
Dk 56, Simba wanapata kona yao ya nne, inachongwa vizuri lakini wmisho Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 55 Muzamiru anaachia shuti kali, mpira unaguswa na kuwa kona, inachongwa, mpira unamfikia Mo Ibra tena, anaachia mkwaju mwingine lakini goal kick
Dk 53 krosi nyingine nzuri ya Bukungu, lakini Mavugo na Manula wanavaana na mwamuzi anasema offside
Dk 52 krosi nzuri inamfikia Mavugo, anashindwa kufunga, unakwenda kwake Kichuya naye anashindwa kufunga na Manula anadaka vizuri
Dk 51, mpira mzuri wa adhabu, anaruka juu Aggrey na kupiga kichwa vizuri, mpira unapita juu kidogo ya lango la Simba
Dk 50, Bocco anapokea pasi nzuri la Gadel, anaachia shuti lakini linakuwa kuuubwa
GOOOOOOOOOOO DK 48, krosi safi ya Mavugo, Mo Ibrahim anajipinda na kuachia mkwaju mkali unaomshinda Manula
Dk 47, Kapombe alitaka kufanya mzaha lakini Manula anaondosha mpira hup
SUB Dk 45 Shabani Iddi anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Frank Domayo, inaonekana Azam FC wameamua kupunguza mshambulizi, kuongeza kiungo kwa lengo la kusaidia kuzuia kuzidiwa katika kiungo. Domayo ni kiungo mlinzi, hivyo sasa Azam FC inacheza na viungo watatu wa ukabaji plus Stephan Kingue plus Himid Mao
MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
DK 44, Simba wanagongeana kwa dakika moja nzima bila Azam kuupata mpira lakini shuti Ajib linapaa juuu
Dk 42, Kichuya anapiga shuti tena lakini ni butu. Kila wanapoingia kwenye lango la Azam FC, Simba wanaonekana kutokuwa na utulivu
Dk 41, Kichuya anajaribu nje ya 18, lakini Manula anaonyesha utulivu kwa mara nyingine
Dk 39 Ajibu anaingia, anapiga krosi katikati ya lango la Azam chinichini lakini Manula anaifuata na kudaka vizuri
Dk 35, krosi nzuri ya Mo Ibrahim, Mavugo anaruka na kupiga kichwa lakini Manula anadaka vizuri na kuanguka chini hapa
Dk 34 krosi nzuri ya Gadiel Michael, Shabani anashindwa kufunga akiwa hatua moja na lango la Simba, anapiga kichwa kinakwenda nje
Dk 31, Mo Ibrahim anaingia vizuri lakini Manula anaonyesha umahiri na kudaka vizuri kabisa
Dk 30, Azam FC wamekuwa wakirudi nyuma wote na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza. Lakini Simba wanaendelea kusukuma mashambulizi mengi na kutawala katikati lakini si makali
KADI Dk 28, Bukungu analambwa kadi ya njano, inakuwa kadi ya tatu ya njano na moja nyekundu katika mchezo huu
Dk 25, krosi safi ya Zimbwe hapa, lakini Manula anapangua na Mao anaosha
Dk 25, Ajibu anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali hapa lakini umeguswa, kona
Dk 22 sasa, Azam F wanaendelea kusukuma mashambulizi na wanacheza vizuri kama hawako pungufu
Dk 19, Azam FC wanapata kona, inachongwa hapa Agyei anadaka, mpira unamtoka na Mkude anawahi na kuondosha
KADI NYEKUNDU....Dk 16, SUre Boy analambwa kadi nyekundu kwa kumuangusha tena Ajibu hapa
Dk 15, Ajib yuko chini hapa na analalama kwamba alipgwa kipepsi
Dk 14 sasa, timu zinacheza kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa uwanja unateleza sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Dk 10, Shabani anampiga chenga Agyei hapa, mpira unabaki kwa Singano yeye na lango hatua mbili tu mbele yake lakini naye anateleza na kuanguka chini
Dk 7, Mo Ibrahim anaingia krosi safi kabisa hapa lakini Mao anaokoa vizuri kabisa, ilikuwa hatari
KADI Dk 6 Mo Ibrahim analambwa kadi ya njano kutokana na kumfanyia madhambi Himid Mao

Dk 4, krosi nzuri kabisa ya Singano, hatari kabisa lakini anawahi Kotei
KADI Dk 3, Aggrey Morris analambwa kadi ya njano kwa mchezo wa kindava
Dk 1, Simba ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Azam FC lakini Manula anadaka vizuri