.
Arsenal wanaamini kwamba huenda
wakapoteza nafasi ya kumnunua mchezaji ambaye wamekuwa wakimtafuta sana,
Thomas Lemar wa klabu ya Monaco.
Hii ni baada ya Monaco kuwauzia Chelsea kiungo Tiemoue Bakayoko.
Mchezaji wao mwingine Benjamin Mendy anatarajiwa pia kuwaaga, jambo ambalo linaifanya vigumu kwao kumuuza Lemar.
Hayo yakijiri, Arsenal wamesalia kufanya kila wawezalo kumzuia Alexis Sanchez kuondoka.
Mchezaji huyo wa Chile anaingia katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake wa sasa katika kalbu hiyo na anadaiwa kutaka kuondoka, lakini Gunners wanataka kumkwamilia
Alikuwa mfungaji bora wao msimu uliopita.
Monaco walimuuza Bakayoko kwa Chelsea kwa £40m, naye beki wa kushoto Mendy anahusishwa na kuhamia Manchester City.
Kuna pia tetesi kwamba mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 18, ambaye pia anatafutwa na Arsenal na Real Madrid anaweza kuondoka.
Arsenal kipindi hiki wamemnunua mshambuliaji Alexandre Lacazette kutoka Lyon kwa £46.5m ambayo ni rekodi kwao.
Walimchukua pia beki wa kushoto Sead Kolasinac kutoka Schalke bila kulipa ada yoyote baada yake kuwa amemaliza kutumikia mkataba wake.