Rodgers alitupiwa virago na Liverpool Oktoba 2015 kufuatia madai kuwa kocha huyo raia wa Ireland hakuweza kutatua matatizo ya beki mbovu iliyokuwa ikiruhusu magoli kizemmbe, na kuigharimu timu kupoteza pointi zaidi.
Klopp aliiongoza Liverpool hadi kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Ku Uingereza msimu uliopita, lakini kiulizo bado kipo kuhusu safu ya ulinzi ya Liverpool, ambayo tayari imesharuhusu magoli tisa katika ligi msimu huu.
"Naam, amewarejesha kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kutinga nafasi ya nne msimu uliopita, jambo ambalo limempa sifa nyingi," Shearer aliandika katika kolamu yake kwenye The Sun.
"Ukweli, ni kwamba, Liverpool haina tofauti yoyote chini ya Klopp zaidi ya ilivyokuwa chini ya Brendan Rodgers, kweli wanakimbia sana mbele, lakini nyuma hawana ujanja."
Liverpool hawajashinda mechi tatu za mwisho katika michuano yote, na walishikiliwa kwa sare ya 1-1 na Burnley kwenye Ligi Kuu Uingereza Jumamosi mchana.