Fashion

Tuesday, 19 September 2017

POMBE YAMFANYA ROONEY KUTOENDESHA GARI KWA MIAKA MIWILI


Nahodha wa zamani watimu ya taifa ya England Wayne Rooney amehukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili sambamba na kufanya kazi za jamii kwa saa 100.


Rooney 31, alikamatwa kwenye kitongoji cha Wilmslow, Cheshire kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa Septemba 1.

Rooney pia atalipa faini ya Pauni 170 kwa kosa hilo.
''Nimekubali kosa langu na nimeomba radhi kwa familia, klabu yangu ya Everton, mwalimu na sasa ni zamu ya mashabiki.Ninaomba radhi kwa kitendo kile.'' alisema Rooney baba wa watoto watatu.
 
Jaji amemwambia Rooney alijiweka yeye na watumiaji wengine wa barabara katika hatari kubwa
Mchezaji huyo aliyezaliwa katika jiji la Liverpool alijiunga na Everton klabu yake ya utotoni akitokea Manchester United miaka 13 baada ya kuondoka.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :