Fashion

Friday 3 November 2017

ARSENAL YAFUZU 32 BORA UROPA LIGUE

 
.
Arsenal walifanikiwa kujikatia tiketi kucheza raundi ya 32 baada ya sare isiyo ya magoli dhidi ya Red Star Belgrade katika uwanja wa Emirates.
 
Washika Mtutu hao walishindwa kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Red Star, lakini sare, ushindi wa Cologne dhidi ya BATE Borisov ukiwavusha hatua ya mtoano.

Arsenal iliyokuwa na mabadiliko makubwa ilimiliki mchezo lakini Richmond Boakye alipoteza nafasi ya muhimu sana kuwapatia Red Star ushindi.

Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Uingereza cha hivi karibuni, Jack Wilshere alikaribia kumpa chakula cha akili Gareth Bale kwa kufunga goli la ushindi, lakini Damien Le Tallec alikoa kuhakikisha wanagawana pointi.

Baada ya kuipatia timu yake ushindi Belgrade wiki mbili kabla, Olivier Giroud alikaribia kuendeleza umahiri wake wa kufunga aliponyooshewa kibendera na mwamuzi dakika ya 10, lakini, baada ya kutengewa pande na Ainsley Maitland-Niles,, shuti lake dogo liliangukia moja kwa moja kwa kipa wa Red Star Milan Borjan.

Kama ilivyotarajiwa, Arsenal walitawa mchezo lakini Red Star ambao walichezewa nusu uwanja waliendelea kuchangamka kadiri muda ulivyoendelea.

Arsenal walikuwa na bahati kwenda mapumziko bila kufungwa baada ya Boakye kupoteza nafasi mbele ya goli.

Iliwachukua Arsenal dakika 65 kufanya jaribio lingine kwenye lango la Red Star kwani Wilshere aliingia eneo la hatari akichukua mpira kutoka kwa Ainsley Maitland-Niles na kupiga kuelekea golini, lakini Le Tallec alizuia.

Arsene Wenger alimgeukia kinda wa miaka 18, aliyefunga mechi ya Kombe la Carabao Eddie Nketiah kutafuta goli lakini nafasi zilimwangukia Theo Walcott, ambaye alichemka mara mbili.

Arsenal watarejea kwenye Ligi Kuu Uingereza Jumapili ambapo watasafiri kwenda Manchester City.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :