Fashion

Saturday 4 November 2017

SINGIDA UNITED 4-4-2 YANGA 4-3-3


Kikosi cha Singida United kesho kitaikaribisha Yanga, kwenye uwanja wake halisi wa Nmfua ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kuutumia uwanja huo tangu ligi ilipoanza Agosti 26, mwaka huu.


Mchezo huo wa kihistoria unatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi kutokana na wakazi wa mkoa huo kutoiona timu yao tangu ilipopanda daraja na kucheza ligi kuu msimu huu, lakini kitu kingine kinachofanya mchezo huo kuwa gumzo ni kikosi cha Yanga kuwa na muda mrefu bila kucheza kwenye mkoa huo.

Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, atakuwa akiwakaribisha vijana wake wa zamani kwa mara ya kwanza tangu alipoachana nao Novemba mwaka jana baada ya kutimuliwa kazi na nafasi yake kupewa Mzambia George Lwandamina ambaye kwasasa ndiyo kocha mkuu.



Hiyo ni mara ya pili timu hizo kukutana mara ya kwanza ilikuwa ni katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, hivyo katika mchezo wa kesho niwazi Pluijm hatikubali kupoteza kwa mara ya pili dhidi ya vijana wake wa zamani.

Timu hizo zinakutana ikiwa zinatofautiana kwa pointi tatu Yanga ikiwa juu  kwenye nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 16, wakati Singida United ikishika nafasi ya tano ikiwa na pointi 13, hivyo kila upande hautokubali kupoteza mchezo huo kwa kuhofia kupitwa au kuondolewa kwenye harakati za kuwania taji hilo.


Yanga tayari imetua mkoani Singida ikiwa na kikosi chake kamili ispokuwa nyota wawe waliokuwa majeruhi Amissi Tambwe, Donald Ngoma,Thabani Kamusoko na Juma Abduli   ambaye anakadi tatu za njano hivyo hatoweza kucheza mechi hiyo.

Kutokuwepo kwa Juma Abduli nafasi yake huenda ikachukuliwa na Hassan Ramadhani Kessy ambaye ndiyo mbadala katika nafasi hiyo na kocha Lwandamina ametamba kuibuka na pointi tatu kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Kama ilivyokuwa kawaida Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wanatarajiwa kuongoza mashambulizi ya Yanga huku Papy Kabamba Tshishimbi na Kelvin Yondani wakianza kwenye safu ya ulinzi ya Yanga ambayo itaendelea kutumia mfumo wa 4-3-3 kama inavyofanya pindi inapocheza na timu yenye viungo wengi.

Kwaupande wake kocha wa wenyeji Hans van der Pluijm, ameapa kuweka urafiki pembeni na kuifunga Yanga timu ambayo amesema yeye ndiyo ameipa mafanikio iliyokuwa nayo hivisasa.

Hans Pluijm anaingia kwenye mchezo huo akiendelea kujivunia kikosi chake hasa safu yake ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Danny Usengimana raia wa Rwanda na beki Shafiq Batambuze ambaye amekuwa na uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi ya timu hiyo.

Katika eneo la kiungo Singida wataendelea kumtegemea Mdathiri Yasini anayecheza kwa mkopo akitokea Azam sambamba na Deusi Kaseke huku katika eneo la golikipa Manyika Peter akitarajiwa kuanzia langoni huku Ally Mustapha Barthez akianzia benchi.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwenye eneo la kiungo kutokana na timu zote mbili kuwa na wachezaji makini wanaomudu vyema kucheza nafasi hiyo ambayo ni muhimu katika timu yoyote katika kutengeneza nafasi.

Singida wanatarajia kutumia mfumo wa 4-4-2, na hiyo ni kutokana na kucheza nyumbani wakiwa na malengo ya kufanya mashambulizi mengi kupitia pembeni ili kupa idadi kubwa ya mabao kama itawezekana.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :