Friday, 29 December 2017
YANGA BILA AJIBU ,CHIRWA USO KWA USO MBAO CCM KIRUMBA
Mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Yanga Ibrahim Ajibu, ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji ambao watasafiri na timu hiyo kesho kuelekea Mjini Mwanza kwenda kuikabili Mbao FC, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa 12, wa Ligi Kuu ya Tanzania bara
.
Msemaji wa Yanga Dismas Ten, amesema kuwa Ajibu hatokuwepo na timu hiyo kutokana na kutumikia azabu ya kadi tatu za njano hivyo analazimika kukosa mchezo mmoja ambao ndiyo huo dhidi ya Mbao FC.
"Timu inaondoka kesho Ijumaa kwa usafiri wa ndege ya Fast Jet kwenda Mwanza tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, lakini tunasikitika kwamba hatutokuwa na washambuliaji wetu tegemezi ambao ni Obrey Chirwa na Ajibu ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali Chirwa akiwa bado yupo kwao Zambia kwa ajili ya matatizo ya kifamilia lakini Ajibu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano," amesema Ten.
Msemaji huyo amesema baada ya hilo kutokea kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa atawatumia washambuliaji Pius Buswita na Amissi Tambwe ambao kwasasa ndiyo wapo fiti baada ya kushiriki mazoezi kikamilifu chini ya kocha huyo msaidizi.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.