Beki huyo wa kati, ambaye alikuwa kipaumbele cha Jurgen Klopp tangu majira ya joto na alishapanga kutua Anfield tangu hapo, atajiunga rasmi na Liverpool Januari mosi.
Mazungumzo yaliendelea kwa kasi baina ya pande mbili baada ya mchakato mrefu wa Reds kutengeneza mahusiano mema na upande wa pili kufuatia tukio lililotokea Juni na kuwafanya Saints kukataa kumuuza mchezaji huyo.