BARCELONA WAPIGA REAL MADRID KAMA WATOTO
Barcelona wameizidi Real
Madrid pointi 14 kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kushinda 3-0
Clasico ya Jumamosi kwenye uwanja wa Bernabeu
Luis
Suarez alianza kufungua ukurasa wa mabao akimalizia pasi ya Sergi
Roberto muda mfupi tu baada ya mapumziko, Lionel Messi akiipatia
Barcelona goli la pili kwa mkwaju ya penalti baada ya Dani Carvajal
kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira uliopigwa na Paulinho.
Real Madrid hawakuweza kujibu mapigo baada ya kupunguzwa watu 10, na
Barcelona walimuingiza Aleix Vidal ambaye aliipatia timu bao la tatu
baada ya Keylor Navas kushindwa kuujaza mikononi mpira dakika za
majeruhi.
Goli
la Vidal lilikamilisha siku chungu kwa kikosi cha Zinadine Zidane,
ambaye matumaini ya La Liga yanaonekana kuzidi kufifia licha ya kuwa na
mchezo mkononi. Barcelona walishangilia ushindi wa tatu mfululizo kwenye
uwanja wa Bernabeu kwa mara ya kwanza katika historia.
Kilikuwa
kipigo cha kudhalilisha kwa Madrid lakini ni wachache tu walioweza
kubashiri ushindi wa mabao 3-0 baada ya kumiliki mchezo kipindi cha kwanza
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.