Sunday, 24 December 2017
NDOA YA JOSEPH OMOG IMEZIMA KAMA MSHUMAA
Klabu ya Simba imemfukuza kocha wake Joseph Omog, baada ya viongozi wa timu hiyo kufanya kikao cha dharura na kufikia maamuzi hayo kwa ajili ya maslahi ya timu.
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameiambia wameamua kuachana na kocha huyo kutokana na matokeo mabaya iliyoipata timu hiyo jana dhidi ya Green Worriors, na kuvuliwa rasmi taji la FA na timu hiyo ya daraja la pili.
"Nikweli tumevunja mkataba na kocha Omog, baada ya makubaliano yapande yenye maslahi kwa pande zote mbili sisi klabu ya Simba, tunamtakia safari njema Omog na siku zote tutaendelea kuutambua na kuuthamini mchango wake kutoka huko tulipoanza naye hadi hapa alipotufikisha," amesema Manara.
Msemaji huyo amesema baaada ya kocha huo kuondoka timu yao itabaki chini ya kocha msaidizi Masud Djuma, ambaye sasa ndiye atakayeiongoza klabu hiyo kwenye michuano yote ambayo inashiriki ikiwepo ile ya Kombe la Mapinduzi huku uongozi ukiwa katika jitihada za kumtafuta mbadala wake.
Omog alikuwa akilalamikiwa kwa muda mrefu na mashabiki na wanachama wa timu hiyo kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo ambayo imesheheni wachezaji mastaa walioigarimu klabu hiyo kiasi cha Bilioni 1.3, katika usajili wao wa msimu huu lakini ilikuwa ni tofauti na matokeo waliyokuwa wakipata uwanjani.
Kufukuzwa kwa Omog kunahitimisha fununu za sikunyingi zilizokuwa zinamuhusu kocha huyo kufukuzwa kwenye klabu hiyo kongwe nchini ambayo haijafanya vizuri kwa misimu minne mfululizo.
Omog ametua Simba mwanzoni mwa msimu uliopita kuchukua nafasi ya Muingereza Dylan Kerr na kwa kipindi chote alidumu Simba aliweza kuisaidia timu hiyo kutwaa
ubingwa wa Kombe la FA, kushuka nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya msimu uliopita na kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na kubeba Ngao ya Jamii msimu huu baada ya kuwafunga wapinzani wao Simba.
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.