Mabingwa Yanga wamepangwa kuanza na St Louis ya Shelisheli katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano ugenini.
Endapo itavuka kikwazo hicho Yanga inatarajia kupambana na mshindi kati ya Township Rollers ya Botswana na El Merreikh ya Sudan na baada ya hapo itafuzu moja kwa moja katika hatua ya makundu ya michuano hiyo mikubwa kabisa Afrika.
Kwaupande wawakilishi wengi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Simbawenyewe wamepangwa kuanza na Gendarmerie Tnale ya Djibouti katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani,
Mechi ya kwanza ikichezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano ugenini Ikivuka hapo, Simba itakutana na mshindi kati ya El Masry ya Misri na Green Bu faloes ya Zambia.