Fashion

Thursday, 8 March 2018

DEMBELE KUONDOKA BARCELONA ENDAPO ITAMSAJILI GRIZMAN



  Mchezaji wa  klabu ya FC. Barcelona, Ousmane Dembele, amesema hana furaha na taarifa zinazoeleza kuwa Kocha wake, Ernasto Valverde, ana mipango ya kumsajili mchezaji Antoine Griezmann kutoka Atlerico de Madrid.


Dembele amesema kama Valverde atamsajili mchezaji huyo, basi ataondoka klabuni hapo na kwenda kucheza soka sehemu nyingine.

Kauli hiyo imekuja kufuatia tetesi ambazo zimeanza muda mrefu kuwa Barcelona inataka kumsajili Mfaransa huyo, ambaye amekuwa tegemeo kubwa ndani ya Atletico Madrid.

Ikumbukwe Dembele alijiunga na wakatalunya hao msimu uliopita wa majira ya joto akitokea Borussia Dortmund kuja kuchukua nafasi ya Neymar Jr aliyeuzwa kwenda PSG ya Ufaransa kwa kiasi cha pauni milioni 200.

Ujio wa Dembele ndani ya Barcelona ulikuwa ni kuchukua nafasi ya Neymar, japo alipatwa na majeruhi mapema tu baada ya kujiunga na timu, lakini ujio wa Coutinho mwezi January uliondoa pengo lake kwa kikosi kuimarika.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :