Na steve sameo
Fainali ya europa ligi imekwisha kwa Sevilla kuibuka kwa ushindi mnono dhidi ya klabu ya Liverpool kwa jumla ya goli tatu kwa moja .
Katika mchezo huo klabu ya Liverpool ndio iliyokuwa ya kwanza kuziona nyavu za klabu ya Sevilla mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Liverpool ilikuwa inaongoza kwa goli 1 lililofungwa na mshambuliaji Sturrige huku Sevilla ikirudi kwa nguvu katika kipindi cha pili na kuandika magoli matatu yaliyotiwa kimyani na Gameiro na Coke aliyerudi kimyani mara mbili.