Na steve sameo
Uongozi wa Azam FC umetangaza kuachana na kocha wake mkuu Stewart
Hall, baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufikia kikao
kilichofikia maazimio hayo
.
Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saada Kawemba amesema
wamefanya hivyo kwa ajili ya kumpa nafasi kocha huyo kuendelea na
mipango yake mingine ya ya kutafuta kazi sehemu nyingine kama alivyosema
anataka kutafuta changamoto sehemu nyingine.
“Tumeamua kumalizana na kocha Hall, kwa makubaliano maalumu ya pande
zote mbili na kuanzia leo Hall siyo kocha wetu na timu yetu itakuwa
chini ya kocha msaidizi Dinnis Kitambi katika mechi zetu mbili zilizo
baki ile ya mwisho ya ligi ya Vodacom dhidi ya Mgambo JKT na nyingine ni
ile ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga ambayo itapigwa Juni
11.,”amesema Kawemba.
Wednesday, 18 May 2016
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.