Fashion

Sunday, 24 July 2016

YANGA KUSUKA AU KUNYOA KOMBE LA SHIRIKISHO






Wakati Yanga imetua salama 
jijini Accra nchini Ghana, Kocha Hans van der Pluijm amesema haitakuwa kazi rahisi dhidi Medeama.

Mechi Yanga dhidi ya Medeama itapigwa keshokutwa Jumanne na Pluijm amesema anajua Medeama watakuwa wamejipanga kweli.

“Watakuwa wamejipanga vilivyo, lakini sisi hatutakubali, tumejipanga na tuko,” alisema Pluijm.

“Tumekuwa na maandalizi ya muda mwingi wa maandalizi na tunaamini tuna uwezo mzuri wa kupambana tukiwa tumejirekebisha.”

Katika mechi ya jijini Dar es Salaam, Yanga na Medeama walitoka sare ya bao 1-1 na wageni wakisawazisha baada ya uzembe wa beki Vicent Bossou. 

Hata hivyo, bado Yanga ilikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi lakini wachezaji wake hasa washambuliaji walikosa nafasi nyingi za kufunga.

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :