.
Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa
ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania
kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya
kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea.
Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.
Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushiriki mechi za kimataifa.
Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.