Fashion

Monday 30 January 2017

WACHIMBAJI WA MADINI WAOKOLEWA WAKIWA HAI GEITA


Wachimbaji madini 15 wameokolewa wakiwa hai baada ya mgodi wao kupolomoka siku tatu zilizopita


Ajili hiyo iliyokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, tarehe 26 Januari, katika mgodi uitwao RZ Gold Mine, unaomilikiwa na raia wa China katika machimbo ya dhahabu yaliyopo Geita Kaskazini Magharibi mwa Tanzania

Manusura hao ni raia 14 wa Tanzania na mmoja wa China.
 aliyeshuhudia zoezi la uokoaji anasema eneo hilo lilijawa na shangwe na vilio vya furaha wakati ndugu, jamaa na wachimbaji wengine walipokuwa wakishuhudia uokoaji wa manusura hao. 


Manusura hao walionokena wadhaifu kiafya, lakini walipatiwa huduma ya kwanza mara moja na kisha kupelekwa katika kituo cha afya kilichopo jirani 

Uchunguzi wa nini hasa kilisababisha ajali hiyo unaendelea, lakini hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea
Mwaka jana mwezi Novemba, Tanzania ilisherehekea ukoaji wa 'kimiujiza' baada ya wachimbaji watano kuokelewa wakiwa hai baada ya kukwama chini ya ardhi kwa siku 41.

Eneo la Magharibi mwa Tanzania lina migodi mingi na wachimbaji wengi hutoka vijiji vya jirani. 



Hata hivyo migodi mingi haikaguliwi mara kwa mara na hali ya usalama ya migodi hii haitimizi viwango rasmi. 

Naibu waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani, amesema serikali itahakikisha wachimbaji wana kuwa salama.

Mgodi huo utakuwa chini ya uangalizi kwa siku tano kabla wachimbaji kuruhusiwa kufanya kazi. 

Naibu waziri pia amewaagiza makamishina wa madini kufanyia tathmini migodi mwingine ya wachimbaji wadogo kwa siku tano, kuanzia kesho

Unknown

About Unknown

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :