Wednesday, 25 January 2017
LIVERPOOL KUSUKA AU KUNYOA LEO EFL CUP
Watazamaji wa EPL, Ligi Kuu England, watapaswa kusubiri hadi Januari 31 ili kupisha Nusu Fainali za Kombe la Ligi, EFL, CUP, ambazo zitachezwa Jumatano na Alhamisi hii na kisha kuanzia Ijumaa hadi Jumapili patakuwepo na Mechi za Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP.
EPL itakuwepo angani Jumanne Januari 31 kwa Mechi 7 na Jumatano Februari Mosi zipo Mechi 3 lakini Jumanne ndio ipo Bigi Mechi huko Anfield kati ya Liverpool na Chelsea.
PATA RATIBA ZA EFL CUP, FA CUP na EPL:
EFL CUP
Kwa vile Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na kwa vile Mechi zake za kwanza zimeshachezwa, hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
Katika Mechi za Kwanza Man United iliifunga Hull City 2-0 huko Old Trafford na Liverpool kufungwa 1-0 huko Saint Mary na Southampton.
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
**Saa za afrika mashariki **Kwenye Mabano Mabao Mechi ya Kwanza
Jumatano Januari 25
2300 Liverpool v Southampton [0-1]
Alhamisi Januari 26
2245 Hull City v Manchester United [0-2
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.