Tajiri kijana zaidi
barani Afrika, Mtanzania Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Kiongozi Bora
Afrika katika hafla iliyofanyika jijini Zurich nchini Uswiss.
Dewji maarufu kama Mo
ameshinda tuzohiyo inayojulikana kwa jina la African Leadership Person
of The Year ambayo hutolewa kwa wafanyabiashara au viongozi wanaofanya
vizuri.
Mo ameshinda tuzo hiyo ambayo ni heshima kubwa kwake kwa kuwa watu kadhaa maarufu walikuwa wakipewa nafasi ya kuitwaa.
Mfanyabiashara huyo ambaye
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MeTL Ltd, hivi karibuni aliweka
dau la Sh bilioni 20 kutaka kununua hisa asilimia 51 katika klabu ya
Simba.
Kabla amekuwa mdhamini na
mfadhiri wa klabu hiyo akiwa msaada mkubwa wakati ikifika hatua ya
makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuing’oa Zamalek.