Kaya 35,360 za wakulima mkoani mbeya tayari
zimeanza kunafaika na pembejeo za ruzuku kwa msimu wa kilimo kwa mwaka 2016/17
ikiwa ni pamoja na mbolea,mbegu bora za mahindi na mpunga.
Akiongea na mwandishi wa gazeti hili katibu tawala
msaidizi anaye shughulikia kilimo Chimagu Nyasebwa alisema mkoa umepokea
pembejeo za ruzuku tani 3536 za mbolea,tani 265 mbegu za mahindi na tani
150 mbegu za mpunga na kudai kuwa zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo unaendelea
mpaka msimu wa kupanda utakapo malizika.
“Tani 3536 za mbolea ni pamoja na mbolea ya kupandia
na mbolea ya kukuzia na zoezi la ugawaji linaenda vizuri na natarajia baada ya
wiki mbili wataalamu wangu waniletee idadi ya wakulima waliyo nufaika na walio
kosa ili tujue namna ya kuwasaidia walio kosa, hivyo hivyo serikali mmemlipia
mkulima asilimia 30”alisema.
Hata hivyo Nyasebwa aliongeza kuwa utaratibu wa utoaji
wa pembejeo ubamedirika ni tofauti na ule ambao wananchi waliozoea hapo
awali,kwani mwaka huu serikali imebadirisha mfumo wa utoaji wa vocha za ruzuku
kwenda kwenye mfumo wa pembejeo za ruzuku mabapo mwananchi hanunui tena vocha.
Kwa upande wake mkulima wa kata ya Simambwe
Wilaya ya Mbeya vijijini Eston Mwaishungu alilalamikia utaratibu uliyofanywa na
serikali wa kubadirisha mfumo wa vocha bila kutoa elimu.
“sisi wananchi uku tupo tumekaa tunasubilia vocha
kumbe utaratibu umebadirishwa na viongozi wetu wa vijiji na kata wamekaa kimya
na kuto elimisha wakulima sasa tutatambuaje kuwa pembejeo hazitolewi kwa vocha
na matokeo yake bei imekuwa kubwa”