Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameongoza zoezi la kuwabakiza klabuni halo wachezaji watatu muhimu.
Wenger ameongoza zoezi la kuwaongeza mkataba mshambuliaji Olivier Giroud na walinzi Laurent Koscielny na Francis Coquelin.
Taarifa zinasema baada ya hao wawili, Arsenal itakuwa na kazi nyingine ya kuhakikisha inawaongezea mkataba vigogo Mesut Ozil na Alexis Sanchez.
Koscielny mwenye umri wa miaka 31, amesaini mkataba mpya hadi mwaka 2020, Giroud mkataba wake utaisha 2019 yaani mwaka keshokutwa na Coquelin amesaini mkataba wa miaka minne na nusu.