Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite aliyeanza kusoma hukumu leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi amesema washtakiwa wana hatia kwa makosa waliyoshtakiwa.
Mahakama imewahukumu Mbunge, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga(CHADEMA) kwenda jela miezi 5.
Mhe Joseph Mbilinyi SUGU alisema ” Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee..!!”....
Wakili wa washtakiwa Boniphace Mwabukusi amesema wanakwenda kuandaa maombi ya dhamana pamoja na kukata rufaa, wamepewa muda wa kuandaa rufaa hiyo na kuiwasilisha Leo.
Sugu na Masonga walishtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba30 mwaka 2017 wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.